SPIKA wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Aksoni,anarajiwa kuwa mgeni rasmi Mbio za Kiswahili za Masafa Marefu (Marathoni) ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani anaadhimishwa kila mwaka ifikapo Julai 7.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar Es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili nchini,Consolata Mushi,akizungumzia maandalizi ya siku ya kiswahili Duniani.

Mushi amesema mbio hizo zinatarajiwa kufanya tarehe 29.6.2024 mkoani Arusha.

“Katika marathoni hiyo kutakuwa na mbio za kilometa 2,Kiloeta 5, na kilometa 21″Amesema

Amesema mbali na mbio hizo kuelekea maadhimisho hayo kunatarajiwa kuwa maenesho ya vitabu ambayo yatafanyika tarehe 03.07.2024 kuanzia asubuhi katika Ofisi za Bakita zilizopo Makumbusho Jijini Dar es Salaam ambapo yataandaliwa na wachapishaji wa vitabu vya kiada na ziada wakishirikiana na BAKITA.

“Kutakuwa na mjadala wa kitaaluma ambapo wanazuoni watazungumza na kujadili uzoefu wa Nchi za nje katika ufundishaji wa kiswahili ambayo itafanyika Tarehe 04 katika ukumbi wa Maktaba Chuo kikuu cha Dar es Salaam katika tukio hili utajumlisha wageni kutoka nchi za Urusi,Ufaransa,Italia”

Hata hivyo,Mushi,amesema tarehe 07,Julai ndio itakuwa siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya kiswahili Duniani,siku ambayo wanatarajia kupata wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi itafanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.