Mwenyeki wa Bodi ya Mtandao wa jinsia nchini(TGNP),Gemma Akilimali,amesema ili bajeti ya mwaka 2024/2025 ikizi matakwa ya watanzania inatakiwa ishirikishe makundi yote.

Akilimali amesema hayo leo mapema jijini Dar es salaam wakati akitoa maoni juu ya Bajeti ya mwaka 2024/2025 inayowasilishwa na Waziri wa Fedha,
Dkt Mwigulu Nchemba Bungeni Dodoma.

Amesema kumekuwa na changamoto kuhusu Bajeti zinazowasilishwa zimekuwa haziki matakwa ya makundi yote.

“Upungufu ambao tunaona ni ushikirishwaji toka chini na jinsi gani wananchi wanapewa kipaumbele”Amesema Akilimali.

Akilimali ambaye ni mwanaharakati wa siku nyingi wa kutetea haki za Wanawake nchini,ameomba Bajeti hii iende kutatuj changamoto zinazomkabili Mtanzania na isiwe ya kisiasa.

Amesema bado Mtanzania anakumbana na Changamoto zinazomkabili na kutaka bajeti ikaenda kutatua matatizo.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi,ametaka Bajeti iliyowasilishwa ijikite katika kutatua changamoto vifo vya Mama na watoto.

Hata hivyo,Liundi,ameitaka Bajeti pia ijikite katika mabadiliko ya tabia ya nchi ikwemo kutokea majanga ya mafuliko na Ukame.