Naibu waziri wa fedha, Hamad Hassan Chande, amezitaka taasisi za fedha nchini kuzingiatia viwango vya bima pindi wanapotoa mikopo kwa wananchi ili kuepuka mikopo chechefu hali itakayosaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi jumuishi nchini

Ametoa Rai hiyo wakati wa halfa ya kuipongeza benki ya biashara ya mkombozi kwa kupanda kutoka dirisha dogo la soko la mitaji na hisa la Dar es salaam kwenda soko kuu ambapo pia amesema serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini ili kusaidia taasisi za fedha za wazawa kukua kwa kasi


Kwa upande wake,Mary Mniwasa, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ameitaka benki hiyo kutoa taarifa ya mafanikio yake kwa jamii ili kuwezesha bei ya hisa zake kuongezeka na hivyo kukuza pato la benki

Naye,Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Respige Kimati, amesisitiza kuwa wataendelea kutanua wigo wa huduma za benki hiyo kwa kuwekeza zaidi katika miundombinbu ya kisasa ili kuwafikia wateja kwa wingi zaidi

Kimati amesema hatua benki mkombozi kutoka soko la ukuzaji wa mitaji la DSE kwenda kwenye soko kuu la uwekezaji kunathibitisha matokeo yenye nguvu ya mageuzi ya utendaji.

“Tunapoelekea kwenye sehemu ya soko lenye ukomavu zaidi tunaendelea kuongeza thamani kwa wanahisa wetu kwa njia ya gawio la pesa na uwekezaji unaotegeneza thamani kulingana na Dira na dhamira”Amesema Kimati