Umoja wa Nchi Wanachama wa Afrika katika mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Uhifadhi Ulinzi na utunzaji wa misitu wamekubaliana hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wameokoa misitu na ardhi takribani hekta Milioni 100.

Hayo yameelezwa Leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki wakati akifungua mkutano uliowakutanisha  Wanachama wa Nchi hizo Afrika ambapo amesema njia hiyo itasaidia kutunza na kulinda mazingira kwa faida ya kizazi kijacho.

Aidha amesema kuwa kati nchi wanachama 55 wa Afrika walioridhia makubaliano haya ni nchi 34 ambapo hadi sasa Tanzania imeshapanda miti hekta Milioni 2 ambayo ni sawa na asilimia 46.

“Nafarijika kama ninaesimamia sekta ya misitu kwa kuona kuwa nchi mbalimbali zinakabiliana na uharibifu wa misitu na Tanzania chini ya Rais wetu Dkt. Samia ameweka afua mbalimbali kuhakikisha kuwa wananchi wake wanatumia nishati safi ya kupikia Ili kulinda mazingira yetu” Amesema Kairuki.

Amesema Sekta ya misitu kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanalinda uharibifu wa uoto wa asili, miti na misitu.

Kwa upande wake Kamisha wa Uhifadhi wa Misitu Tanzania Prof.Dosantos Silayo amesema Dunia imeweka lengo la kukomboa ardhi ya Tanzania katika kuchangia utunzaji wa mazingira ikiwemo misitu.

Aidha amesema Dunia imeweka lengo la kukomboa Milioni 350 ambapo kwa nchi za Afrika wameweka lengo la kulinda hekta takribani Milioni 100.

Hata hivyo amesema Tanzania katika kuhakikisha kuwa inakomboa ardhi ikiwemo misitu imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa marekebisho ya sera, sheria na kanuni katika kutunza rasilimali za misitu