Ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki imetaarifu kuwa habari zinazo sambaa mitandaoni tangu juzi kuhusu Mh. Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nasary kujivua Ubunge na Kujiunga na ccm siyo za kweli.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Ofisi ya Mbunge Jimbo la Arumeru Mashariki Bw. Julius Ayo imeeleza kuwa Mbunge Nasary hayupo hapa nchi kwa sasa.

“Mbunge Nasari hayupo hata Nchini kwa sasa Yuko Marekani akishunglikia Mambo ya wanachi wa Jimbo lake
Kwa sasa puuzeni habari zinazo sambazwa na wajinga wachache wasio na kazi.”Imesema taarifa hiyo.

03:30