Baadhi ya Watanzania wanakumbana na Changamoto ya kutopata huduma Bora za Afya kutoka na hali ya kimaisha inayosababishwa na kushindwa kuchangia chochote ili kununua kadi ya bima ya Afya ili wawe na uhakika wa kupata matibabu.

Hayo yameyasema leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Dini mbalimbali (ISCEJIC) Askofu Stephen Munga katika mdahalo wa Kamati ya viongozi wa Dini mbalimbali kuhusu haki za kiuchumi na uadilifu wa uumbaji ulioandaliwa na Policy Forum ambapo amesema asilimia 32 yawtanzania ndio wenye bima huku 68 wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma ya Afya kwa kukosa bima.

Aidha ameongeza kuwa jukwaa la viongozi wa Dini mbalimbali wameamua kuiunga Serikali mkono kwa kuwashawishi waumini wao kujiunga na bima za Afya ili wawe na uhakika wa matibabu na kuepukana na changamoto ya kucheleweshewe kupata huduma kutokana na kukosa fedha .

Kwa upande wake Katibu Mkuu Baraza la waislamu Tanzania (BAKWATA) Jabir Mruma amesema Serikali iongeze ufanisi na ushirikiano na sekta binafsi katika Afya hasa ufikiwaji wa huduma za Afya katika maeneo yote mjini na vijijini.

Naye Meneja mradi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Godilisten Moshi amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa Afya ndio jambo la msingi hivyo wajiwekee desturi ya kuchangia huduma za Afya ili kuokoa maisha yao kuliko kwenye masuala mengine kama misiba.

Hata hivyo wameishauri Serikali kugharamia kwa kiasi kikubwa bima kwa kuweka mkakati mzuri wa ukusanyaji wa mapato ili kupata shilingi bilioni 150 kwa miaka 5 ili kugharamia bima ya Afya kwani asilimia 28 ya Watanzania ambao ni wastani wa kaya milioni 2.7 ni za kipato duni