Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kimepata viongozi wapya baada ya kufanya uchaguzi wake Agosti 15 mwaka huu ambapo walifanikiwa kumpata mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina pamoja na wajumbe 6 wa kamati tendaji.

Uchaguzi huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam nakuhudhuriwa na wanachama wa DCPC 72 walimchagua Bi. Irene Mark kuwa Mwenyekiti wa DCPC, Makamu wake Chalila Kibuda, Katibu Hussein Siyovelwa, Katibu msaidizi Fatma Jalala na Mhazina Patricia Kimelemeta.

Akitangaza washindi hao msimamizi wa uchaguzi Mwanasheria Aretas Kyara amesema viongozi wa DCPC wamechaguliwa na wanachama wenzao kwa kuzingatia taratibu na miongozo ya katiba ya Chama hicho na kwa uwazi.

Aidha Mwanasheria Kyara amewatangaza pia washindi 6 wa nafasi za Kamati tendaji ambao ni Wajumbe Shaaban Matutu, Cecilia Jeremiah, Muchunguzi, Christina Gauluhanga, Tausi Mbowe na Selemani Msuya.

Awali kabla ya uchaguzi wanachama wa DCPC walipatiwa semina toka Mfuko wa Bima wa Taifa na Afisa Biasahra wa NHIF Hipoliti Lello ambapo amesema bila wanachama shirika hilo halitoweza kufanya kazi kwani linategemea michango ya wanachama katika kutoa huduma bora kwao.

Aidha amesema Kadi ya Bima ya Afya ni muhimi kwa kila mtanzania katika Kupatana huduma bora za afya ambapo NHIF imegawanya huduma zake katika viwango tofauti ili kila mtanzania aweze kupata huduma hiyo ikiwemo vifurushi vya bima kwa watoto familia wanafunzi mtu mmoja mmoja na waandishi.

Hata hivyo amesema mwanachama mwenye kadi ya bima anauwezo wa kupata Matibabu kwa vituo vyote vya Afya binafsi na serikali zaidi ya 700 isipokuwa matibabu ya nje ya nchi.

Bw. Lello amesema NHIF bado inaendelea kuboresha huduma zake na inapokea changamoto zote za wateja wake wanazokumbana nazo ili waweze kuzitatua kwa wakati.

Kwa niaba ya viongozi wengine wa DCPC Mwenyekiti Irene Mark amewashukuru wanachama wote kwa kuwaamini nakuwachagua kushika nafasi hizo hivyo watahakikusha wanafanya kazi kwa juhudu ikiwemo kuwaunganisha wanachama wote kuwa na umoja na kuwaletea maendeleo.