Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija ametoa maagizo kwa Mkandarasi wa Barabara ya Tabata Kimanga kufika ofisini kwake na mpango mkakati wa ujenzi wa barabara hiyo ambayo imetelekezwa kwa muda mrefu.

Mkuu wa Wilaya Ludigija ameyasema hayo katika ziara yake endelevu ya kukagua miradi ya maendeleo halmashauri ya Ilala ikiwemo miradi ya DMDP ya jimbo la Segerea na Jimbo la Ukonga .

“Dhumuni la ziara yangu kukagua miradi ya maendeleo iliyopo halmashauri ya Ilala nimekuta ujenzi wa barabara hii ya Kimanga ujenzi wake sijaridhishwa nao nakuagiza Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala andika barua ya wito Ijumaa uje na mpango mkakati wa ujenzi wa barabara hii ,pia aseme kwanini amekwamisha ujenzi kwa muda mrefu kupelekea kero kwa Wananchi ” amesema DC ILALA Ludigija

Amemwomba Mkandarasi huyo kufika Ofisi ya Wilaya ya Ilala na ujenzi wake uanze mara moja kuondoa kero hiyo.

Wakati huohuo amepongeza ujenzi wa miradi ya DMDP ikiwemo soko la Bombom ambapo alitoa agizo Soko la kisasa Bombom likabidhiwe Manispaa ya Ilala Mwisho wa mwezi huu wafanyabiashara waanze kazi ndani ya soko hilo .

“Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala naomba simamia wafanyabiasha walengwa wa Kiwalani Bombom Agosti 30 Mwaka huu waanze biashara katika soko lao kila mmoja akikisha anapata kizimba chake ” alisema .

Katika hatua nyingine amepongeza ujenzi wa daraja la Ulongoni A unavyoendelea ambapo unajengwa na mradi wa DMDP amemtaka Mkandarasi kuongeza kasi usiku na mchana kabla mvua za mwezi Octobar kuanza .

Amesema ujenzi wa daraja hilo ukikamilika utaondoa kero kwa Wakazi wa Gongolamboto na Ulongoni ,amepiga marufuku wananchi kuchimba mchanga katika bonde la Mto Msimbazi,amezitaka Kamati za Mazingira kuanzia ngazi ya kata na Manispaa kuachukulia hatua wananchi wenye tabia ya kuchimba mchanga katika bonde la Msimbazi halmashauri ya Ilala