BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali linatarajia kufanya uchaguzi wake wa kupata wajumbe kwenye ngazi mbalimbali hapo Mei 21 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa kamati ya mpito ya kuratibu Uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali,Christina Kamili Ruhinda,amesema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa kanuni ya 5(a)(iv),5(b)(ii) na 5(c) (v) ya kanuni za uchaguzi za mwaka Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2016,Baraza linatakiwa kufanya Uchaguzi kila baada ya miaka mitatu huku uchaguzi awali ulifanyika june 2021.

Ruhinda,amesema kamati yake inawataka mashirika yasiyo ya Kiserikali na umma kwa ujumla kuhusu kuanza mchakatato wa Baraza hilo kufuata ratiba na mambo muhimu kuhusu Uchaguzi huo kupitia kwenye tovuti.

“Kamati pia inatoa wito kwa Viongozi na Wanachama wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi wa Baraza kuanzia ngazi za Wilaya,Makundi maalum,mkoa hadi Taifa”