Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) imebainisha kuwa itaendelea  kushirikiana na wadau wa sekta binafsi nchini katika kuboresha asoko la bima sambamba na kuzuia udanganyifu katika sekta hiyo hali itakayosaidia kuongeza ufanisi wa huduma hizo kwa wananchi wengi zaidi nchini

Pia,TIRA imesema itahakikisha sekta ya bima inaongeza kwenye kuchangia pato la serikali toka asilimia 2 mpaka kufikia asilimia 5.

Hayo yamebainishwa mapema leo jijini dar es salaam na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware wakati wa uzinduzi wa  mpango wa wa utoaji wa dhamana kwa ajili ya ada ya shule (ADABIMA)  pamoja na mpango wa utoaji wa dhamana kwa watelanwalioko katika saccos na vikundi vywa huduma ndogo za fedha

Kadhalika amewataka watoa huduma za fedha na bima nchini kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kutoa huduma bora za bima huku akiwataka wananchi kuendelea kutumia huduma hizo ili kuwa na ustawi endelevu katika jamii.

Kwa upande wake kaimu mtendaji mkuu wa benki ya TCB Jema Msuya amesisitiza kuwa lengo la kuja na mpango huo ni kutoa uendelevu wa elimu kwa watoto ikiwa wazazi watapata maanga ya kifo ama ulemavu wa kudumu na kumfanya ashindwe kulipa ada ya shule


Naye mkuu wa kitengo cha bima kutoka TCB Francis Kaaya amebainisha kuwa mpango huo utasaidia watoto kufikia malengo yao kimasomo ikiwa wazazi wao watapata majanga .
“Tunaelewa umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii yetu.Bima hii inawapa usalama wa kitengo cha fedha lakini pia inalea watoto”Amesema kaaya

Kwa upande wake. Afisa Mkuu Idara ya Fedha,Metro Life Assuarance,Clifford Mkandala amesema wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na SACCOS pamoja na Vikundi vya huduma ndogo za kifedha katika kuimarisha Uchumi na jamii yote nchini.