Msaanii wa Mziki wa Bongo flava Staa Harmonize  May 25,2024 anatarajia kuzindua album yake ya tano katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambayo ameipa jina la ‘Muziki wa Samia’


Msanii huyo amesema lengo ni kupongeza na kuunga mkono kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake.

Ameongeza kuwa album hiyo ni ya mwisho kwake na kusisitiza kuwa ameimba sana kuliko kawaida na ametengezeneza nyimbo 10 ambazo zote zinamlenga Rais Samia hivyo baada ya album hiyo atapumzika na kurefresh huku akiwa anaachia wimbo mmojammoja na sio album tena.

Hata hivyo amesema siku ya uzinduzi huo itakuwa ni usiku wa mialiko na hakutakuwa na viingilio “Tumekusanya mazuri yote ambayo yanafanywa na Rais Samia na Serikali na kuyaweka kwenye kitabu kimoja cha kumbukumbu ambacho kitaishi milele kinachoitwa Muziki wa Samia”