WAZIRI wa nchi,Ofisa ya Rais,Mipango na Uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo, anatarajia kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa jarida la vinywaji vya heiken linalotarajiwa kufanyika May 25 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi habari mapema leo Jijini Dar es Salaam,Meneja Mkazi nchini wa Kampuni ya HEINEKEN,Obabiyi Fagade amesema mbali Waziri Mkumbo katika uzinduzi wanatarajia kuwepo viongozi mshuhuri,viongozi wa tasnia mbalimbali na wawakilishi wa vyombo vya habari kuadhimisha tukio hilo muhimu kwa kinywaji cha Heinek Tanzania.

“Ununuzi wa hivi majuzi ambao umeongeza zaidi ya Euro bilioni 1 katika mapato halisi na Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji kwa nyayo zetu na Afrika bila shaka utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchuml nchini Tanzania,Tumepewa nafasi ya kipekee sio tu kufikia hadhira pana zaidi kutokana na upanuzi huo,lakini pia kutengeneza nafasi nyingi za kazi na kuwawezesha Watanzania”Amesema Fagade.

Hata hivyo Fagade,amesema kwa sasa  Heineken inapatikana katika Masoko 114 na kuuzwa katika masoko 180 na iko tayari kuwa kiongoza katika soko katika tasnia ya vinywaji nchini Tanzania.

Kwa Upande wa Meneja Masoko wa Heineken nchini, Lilian Pascal amesema kuwa Heineken kwa sasa inapatikana katika masoko 114, na kuuzwa katika nchi zaidi ya 180 ikiongoza katika tasnia ya Vinywaji nchini Tanzania.


Amesema kutokana na uwepo wa masoko mengi zaidi lakini wataendelea kuvumbua na kupanua wigo wa jalada lake ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wake.