-Atoa salamu za Mkoa,asema utulivu ulioko katika Mkoa unatokana na viongozi wa Dini

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 17,2024 ameshiriki swala ya Eid Al-Adha Kitaifa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Kinondoni Jijini humo ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa.

Akitoa salamu za Mkoa huo RC Chalamila amesema Mkoa huo ni shwari sana, utulivu tunaouona unatokana na nguvu kubwa za maombi, umoja, upendo na mshikamano ambao unajengwa na viongozi wa Dini

Aidha RC Chalamila amesema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa ili kuweza kupata viongozi wazuri kwa masilahi mapana ya maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla

Hata hivyo RC Chalamila amesema “Tukiona Viongozi wa Dini Tunajivunia Sana” hivyo rai yake kwa vingozi wa Dini kuendelea kushikamana na Serikali katika nyakati zote

Mwisho Baraza hilo la Eid Al Adha Kitaifa limefanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania