MGOMBEA wa Nafasi ya Uenyekititi Taifa wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo amesema akichaguliwa kwenye nafasi hiyo kipaumbele chake ni kuhakikisha anapambana na hali ngumu ya Maisha anayodai inawakumba watanzania.

Doyo ameyasema hayo leo mapema jijini Dar es Salaam wakati akirudisha fomu kwenye ofisi za chama hicho Buguruni jijini hapa.

“Watanzania wanahali ngumu ya maisha ,vitu vimepanda bei,nikipata nafasi hii nitakuwa mstari wa mbele kuwatetea watanzania”Amesema Doyo.

Hata hivyo,Doyo amezungumzia mikopo ya wanawake ambayo amesema imekuwa ikiwaumiza wanawake nchini kwa kufilisiwa mali zao.

“Mimi nimeezunguka mikoani nimeona watanzania wakiumizwa na mikopo umiza,nikipata nafasi nitahakikisha sheria ya mikopo inabadilishwa ili waweze kusaidiwa”Amesema Doyo.