Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wameombwa kufunga maduka yao na kuendelea na biashara na changamoto wanazolalamikia wakutane meza ya mazungumzo wazimalize.

Hayo yameelezwa leo Kariakoo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila baada yakutembelea maeneo ya Soko la Kariakoo ambapo maduka mengi yamefungwa ambapo amesema anatamani kufanya vitu mezani kwa mazungumzo na sio Kwa Shinikizo la wafanyabiashara.

“Wapo wafanyabiashara wanaotaka kufungua biashara zao ila wapo wanaowatishia hivyo niwahakikishie usalama wake wanaotaka kufungua biashara waendelee na sisi tutawalinda na wanaowatishia tutawawajibisha, migomo sio suluhisho” Amesema RC Chalamila.

Aidha amesema kuwa malalamiko makubwa wanazolalamikia ni kuondolewa kwa Machinga kariakoo, wachina wanaouza kariakoo na kupunguza kwa tozo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wadogo Machinga Yusuf Namoto Yusuf amesema malalamiko mengi yanayolalamikiwa na wafanyabiashara hao ni ya kisheria ambayo utatuzi wake utachukua mda.

“Madai hasa hayajulikani ni nini kwani mengi walishakutana na Viongozi wakayaongea yanafanyiwa kazi ila kwa sasa Kuna vipeperushi vinavyosamba havionyeshi anuani ya muhusika hivyo ni ngumu kujua umuulize nani akupe haswa wanachotaka” Amesema Namoto.

Hata hivyo amesema kitendo cha kufunga maduka kinayumbisha uchumi wa nchi na kupoteza wateja hivyo ni vyema wakafungua maduka na kukaa mezani kwa mazungumzo.