Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo Martini Mbwana baada ya kutoa mrejesho wa kikao chao na serikali kwa wafanyabishara amesema ni juu yao  kufunga au kufungua maduka na Polisi wajibu wao ni kulinda biashara zao tu na sio mawazo yao.

Akizungumza leo Kariakoo Jijini Dar es Salaam  leo katika mkutano uliowakutanisha Wafanyabishara hao  ikiwa ni siku 3 tangu wagome kufungua maduka yao wakilalamikia Mamlaka ya mapato TRA kuwakandamiza na toza, kodi na faini ambapo imesababisha baadhi ya wateja wao kuhama na baadhi yao mitaji yao kuelekea kufilisika.


“Niseme ukiona mfanyabiashara amefunga duka lake na kuamua kukaa nje ujue amevurugwa hivyo isitumike nguvu kubwa kwa kutumia maneno makali kinachotakiwa ni kuka meza moja na kuzungumza kujua tatizo linalosababisha hadi akachukua maamuzi magumu hivyo hii ni mara ya pili hali hii kutoke na tukaahidiwa lakini haikutekelezwa na sasa hivyo tunaomba Serikali ifike mahali Kodi zote zitozwe kwa pamoja na ziishie bandarini wakishindwa kutekeleza haya sisi hatutohusika tena” Amesema Martini.

Aidha amefafanua kuwa mwaka huu walikaa kikao Anatoglo lakini hakuna muafaka aliishia kuitwa mara nne kituo cha polisi kuhojiwa lakini hakukata tamaa kudai haki na kile wanachotendewa hivyo sasa kikao alichoitiwa Dodoma wamekaa meza moja na kuzungumza na ahadi imetolewa kero zao zinakwenda kutatuliwa hivyo amewaachia Wafanyabiashara hao uamuzi wa kuamua kufunga maduka au kufungua ni juu yao kwani funguo humiliki wao.

Hata hivyo baada ya mrejesho huo wafanyabiashara wameonyesha kutoridhika na majibu hayo huku wakiendelea kuhoji Kwa nini malalamiko yao hayapatiwi ufumbuzi wa kudumu.