Benki ya EQUITY imezindua kampeni ya ‘HapoHapo’ yenye lengo la kuhakikisha Kila mtanzania anafikiwa na huduma za Benki hiyo hali itakayosaidia kuchagiza ukuaji wa uchumi jumuishi nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo Cha Malipo- Benki ya  EQUITY, Haidari Chamshama amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasiaha ufunguaji wa akaunti kwa njia ya kidigitali ambapo mteja yoyote wa EQUITY atapata huduma hizo kwa njia ya simu yake ya mkononi.

“Tunataka kila mtanzania aweze kufungua awe na Akaunt ya Benk,sahivi haina haja kutembea na makalatasi ili uweze kufungua akaunt ,ni simu yako huku ulipo unaweza kufungua akaunti sharti laini yako iwe imesajiliwa na NIDA”Amesema Chamshama.

Aidha,Chamshama,amesema Benki hiyo kwa sasa inafanya vizuri kutokana na kuwa na huduma bora na kabambe.

Kwa upande wake Meneja wa benki ya Equity tawi la Mbagala Salum khalfani,  ameushukuru uongozi wa Benki kwa kurahisisha huduma hizo ambapo ametoa Wito kwa wakazi wote wa mbagala kuweza kufungua account kwa kutumia simu zao za mkononi

Nao baadhi ya wateja wa benki hiyo akiwemo Theresia Ruziga wamesema huduma hiyo itawarahisishia kupata huduma za kibenki kwa wakati na kuondokana na kupanga foleni wakati wa kuhitaji huduma hizo.