MKURUGENZI wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HELSB), Dkt Bill Kiwia, amesema hali ya urejeshwaji mikopo kwa wanufaika nchini inaridhisha ambapo sasa wanapokea bilioni 15 kwa mwezi toka bilioni 2.5 mwaka 2016.

Dkt Kiwia,ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuwafichua wanufaika wa mikopo ambao wapo mtaani wasiotaka kurejesha Mikopo hiyo, kampeni hiyo iliyopewa kauli mbiu ” kuwa hero wa Madogo”

“Mwaka 2016 tulikuwa tunakusanya bilion 2.5 kwa mwezi,lakini kwa sasa hali ni nzuri tunakusanya Bilioni 16 kwa mwezi toka kwa wanufaika laki mbili wa mikopo hiyo”Amesema Dkt Kiwia.

Aidha,Dkt Kiwia,amesema kwa sasa Tanzania inashika nafasi nzuri Barani Afrika kutokana na hali nzuri ya urejeshwaji mikopo.

Akizungumzia Kampeni hiyo,Dkt Kiwia,amesema kampeni hiyo ya awamu ya kwanza na itadumu kwa miezi miwili itawapa nafasi wananchi kwa watanzania kuwataja wanufaika ambao wapo mitaani ambao hawataki kurejesha mikopo hiyo.

“Kama unamuona mtu unamjua amenufaika unaweza ukataja jina lake,eneo analofanyakazi,chuo alichosoma kwenda kwenye namba 0736665533″Amesema Dkt Kiwia.

Kwa upande wake,Mkurugenzi urejeshaji na urejeshwaji wa mikopo CPA George mzirayi, amesema katika kampeni hiyo wanatarajia kuwafikia Wanufaika zaidi ya elfu hamsini huku wanatarajia kukusanya zaidi ya bilioni mia mbili.