Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka Watanzania kutokuwa nyuma badala yake wametakiwa kujiweka teyari na fursa mbalimbali zinazotokana na uwekezaji mkubwa unaowekezwa hapa nchini

Rai hiyo imetolewa mapema leo Jijini Dar es Salaam Katibu mtendaji wa NEEC, Bibi Being’i Issa,wakati wa Kongamano la nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na Uwekezaji.

Bibi Issa,amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassani,amefungua fursa ya wawekezaji kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza hapa nchini kuwa ni fursa kwa Watanzania.

“Rais ameleta fursa nyingi sisi wote tumeshuhudia wawekezaji wengi wanamiminika kuja nchi na sisi tujipange kwa ajili ya kupata fursa hizi watu wasikae nyuma”Amesema

Hata hivyo,Bibi Issa,amesema wao Baraza wanaangalia wawekezaji wanataka nini  ambapo namna iliyopo sasa ni kuangalia  matakwa ya wawekezaji hao.

Akizungumzia suala nzima la uwekezaji nchini,Bibi Issa,amesema hali ya uwekezaji imeongezeka nchini huku idadi ya watanzania walioajiriwa katika miradi ikiongezeka.

“Jumla ya watanzania laki moja na sitini na mbili kwenye miradi mbalimbali hapa nchini,pia yapo makampuni ya Kitanzania Elfu tatu na sitini yamepata kazi kwenye hii miradi ya kimkatikati hapo Nyuma haikuwepo hivi,haya ni mafanikio makubwa”

Kwa upande wake msimamizi wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP),Said Kipangwa,amesema mradi huo umeweza kuwanufaisha watanzania kwa kutoa ajira lukuki.