KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia  Foundatio yao wamesaini na Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), kwa makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni  udhamini  wa Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika Jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 13, mwaka huu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, iliyofanyika leo Mei 21,2024, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge, amesema kiasi hicho cha fedha kimeongeza chachu ya ushiriano wa pamoja wa kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi.

Aidha, katika kufanikisha Wiki ya AZAKi, FCS wamechangia shilingi milioni 250, ambapo michango mingine inatoka kwa wadau wa maendeleo zik
Shirika la The Foundation for Civil Society (FCS), na  Vodacom Tanzania Foundatio wamesaini makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni  udhamini  wa Wiki ya AZAKI 2024, itakayofanyika Jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 13, mwaka huu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, iliyofanyika leo Mei 21,2024, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge, amesema kiasi hicho cha fedha kimeongeza chachu ya ushiriano wa pamoja wa kukuza maendeleo ya jamii kupitia Wiki ya AZAKi.

Aidha, katika kufanikisha Wiki ya AZAKi, FCS wamechangia shilingi milioni 250, ambapo michango mingine inatoka kwa wadau wa maendeleo zikiwemo asasi za kiraia.

Rutenge amesema kuwa ili kuweza kusonga mbele sauti mbalimbali za wadau na wabia zinahitaji katika kuchochea mchakato wa maendeleo.

“Ili tuweze kusonga mbele na kuiona Tanzania tunayoitaka, sauti za wadau na wabia mbalimbali zinahitajika kusikika na ziwe sehemu ya kutoa mchango katika mchakato mzima wa maendeleo ambayo yatasaidia kujenga maono ya kulipeleka Taifa letu mbele” amesema Rutenge.

Ameeleza kuwa Sekta Binafsi ni wabia na wadau wakubwa wa maendeleo, nakwamba ushirikiano huo ni muhimu katika kubadilishana uzoefu huku akibainisha kuwa FCS wamekuwa wabobezi na wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ushirikiano huu utasaidia kubadilishana uzoefu, Vodacom Foundation watanufaika na uzoefu tulionao katika kusimamia miradi ya maendeleo, kuchochea usawa wa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wanawake, vijana, watoto na watu wenye ulemavu. FCS nao watanufaika katika kuunganisha watu kwa kutumia teknolojia kwa kuzingatia nchi ipo kwenye mapunduzi ya teknolojia” ameeleza Rutenge.