RAIS SAMIA MGENI RASMI BARAZA LA AMANI .


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeaminiwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ambapo katika maadhimisho hayo ya miaka 20 tanayotarajiwa kufanyika Mei 25,2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa kimataifa ambapo mwenyekiti wa Mkutano huo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

Tanzani kuwa nchi mwenyeji imepewa jukumu kubwa la kusimamia shughuli zote zinahusu Baraza, ikiwemo kufuatilia kwa karibu hali ya ulinzi na usalama kwenye Bara la Afrika kutoa miongozo ya kushughulikia masuala ya kiusalama pale inabidi; na pia kuandaa ratiba na kuongoza vikao vya Baraza.


Amebainisha hayo Jijini Dar es salaam Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba amesema Hayo ni majukumu makubwa; na bila shaka Tanzania kuaminiwa na kukabidhiwa ni kutokana na heshima kubwa iliyonayo Barani Afrika na duniani hivyo fursa hiyo ni kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuimarisha Diplomasia ya nchi na kuiongoza kutoa kipaumbele kwenye masuala ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika na duniani .

Waziri Makamba amefafanua kuwa mwezi Machi mwaka 2022, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilichaguliwa kuhudumu kwenye nafasi ya Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa miaka miwili hadi mwezi Machi 2024 ambapo muda wa kuhudumu ulifikia kikomo hivyo Wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Mkutano wa Baraza la Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Februari 2024 Jijini Adiss Ababa, Ethiopia Tanzania ilichaguliwa tena kuhudumu kwenye Baraza hilo kwa muhula mwingine wa miaka miwili hadi mwaka 2026