Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea wawekezaji 25 kutoka nchini Qatari kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha TIC Anna Lyimo amesema wawekezaji hao wamelenga Sekta ya mifugo, uzalishaji wa vifaa tibaa, madawa Utalii usafiri wa anga pamoja na uchumi wa blue.

Aidha amesema Kituo cha TIC kimewakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta hizo wanazotaka kuwekeza ili waweze kupatiwa taarifa muhimu zitakazowawezesha kujua fursa zilizopo hapa nchini.

Aidha amesema wawekezaji watatembelea Zanzibar nakupokelewa na kituo Cha uwekezaji kuangalia fursa zizopo na wanatarajiwa kuondoka nchini tarehe 29.

Hata hivyo amesema tangu mwaka umeanza kumekuwa na kasi ya uwekezaji kuongezeka kwani wamepokea wageni mbalimbali kutoka nchi tofauti Duniani.

“Mwamko wa uwekezaji kutoka nje umekua mkubwa kutokana na awamu ya sita kufungua milango katika masuala ya uchumi na uwekezaji na wengi wao wameonesha nia ya kuwekeza katika miradi ya watu binafsi na Serikali”Amesema Bi Lyimo.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani wasisite kwenda kutembelea vituo vya Kanda na tovuti ya kituo cha uwekezaji Tanzania kupata taarifa, ili waweza kujua wageni gani wamefika na wanataka kuwekeza katika maeneo gani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi ya Taifa Dkt. Peter Msophe amesema kuwa wapo tayari kufanya uwekezaji wa pamoja na wawekezaji wa nchini Qatari, huku akikishukuru kituo cha uwekezaji kwa kuwainganisha na wawekezaji.

Amesema kuwa, kampuni ya Ranchi ya Taifa inashughulika na uzalishaji, uchakataji na uuza wa mazao ya mifugo hasa upande wa nyama, mbuzi, Ng’ombe na kondoo na bidhaa za ziada kama majani na mbolea.

Aidha, amesema kuwa, kutokana na ziara waliofanya kwenye maonesho ya kilimo yakifanyika nchini Qatar yamezaa matunda ambapo leo wawekezaji wa nchini Qatar wamefika Tanzania kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na kuangalia fursa zilizopo.

“Wiki mbili zilizopita tulienda kuiwakilisha Serikali yetu katika maonesho makubwa ya tisa ya kilimo na Mazingira yaliyofanyika Doha nchini Qatar, ambapo ndio leo ziara ile imezaa matunda hayo”amesema Dr Msophe.

Ameongeza kuwa, kati ya mambo makubwa yaliofanywa na TIC, ni kuandaa huu Mkutano huo kati ya viongozi wa qatar na watanzania Ili kukutanisha ni fursa kubwa nchi Tanzania kuweza kupata nafasi ya kupeleka mazao yetu ya kilimo na biashara na tayari mazao ya mifugo yameanza kuliwa nchini Qatar.