TATIZO la ukosefu wa Ajira na kutojiamini ni miongoni mwa matatizo yanayotajwa kumrudisha nyuma mwanamke kuweza kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamebainishawa na Mkurugenzi wa taasisi ya Young women Entrepreneurship, Dkt Jesca Mkwabi, wakati mkutano uliowashirikisha wanawake kutoka sekta mbalimbali yenye lengo kutoa tuzo kwa wanawake 50 waliofanya vizuri kutoka sekta mbalimbali.

“Watu wanamaliza vyuo wanakosa kazi wapo wengine wakikosa kazi hawajishughulisha biashara na kukosa kujiamini pia kwa wanawake kujaribu fursa mbalimbali haya yanachangia kurudisha nyuma harakati wanawake”Amesema Dkt Mkwabi.

Aidha,Dkt Mkwabi ametumia mkutano huo kupitia taasisi yake kuwashauri wanawake kujishughulisha kibiashara na kuacha kuitegemea serikali.

Kadhalika,Dkt Mkwabi amewaomba pia wanawake waliofanikiwa ambao wapo katika sekta mbalimbali nchini kutumia nafasi hizo kutoa elimu kwa wanawake ambao hawajafanikiwa ili nao waweze kujikwamua.

Akizungumzia dhumuni la mkutano huo,Dkt Mkwabi,amesema kwa miaka miwili sasa wamekuwa wakitoa tuzo kwa wanawake 50 kutoka sekta mbalimbali hasa wenye umri wa miaka 20 mpaka 35 ili kuwapa nguvu ili waweze kufanya vizuri katika kazi zao ili waweze kuwavutia wengine.

Kwa upande wake wanawake waliopata tuzo ,wameipongeza taasisi hiyo kwa hatua ya kuwainua wanawake nchini huku wakiwataka wanawake wengine kujitokeza katika kutokaa nyuma kujitokeza katika mikutano kama hiyo.