Benki ya KCB Tanzania imebainisha kuwa itaeendelea kuwainua vijana kupitia programu yake ya 2jiajiri ambapo hadi sasa vijana 500 wanasomeshwa jiji Dar es Salaam ambao wanatarajia kumaliza mafunzo yao mwaka huu.

Takwimu za Benki hiyo inaonyesha kwamba, wanafunzi hao wanapomaliza mafunzo kupitia programu hiyo, wanakua na uwezo wa kuanzisha kampuni na kuajiri wenzao.

Mkuu wa Kitengo cha KCB Sahl Banking kinachotoa huduma za kibenki zinazingatia misingi ya Shariah, Amour Muro ameyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la Ramadhani la Hay-atul Ulamaa lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Aidha,Muro Amesema Hadi sasa wamefanikiwa kuwafikia vijana zaidi ya 1780 na lengo ni kufikia vijana 5000 .

“Tumeona kwamba kuna wengine wanashindwa kuzifikia huduma hizi huduma kwakuwa bado hawajatimiza vigezo vya kuweza kuhudumia na bank, hivyo katika kuwainua vijana tukaanzisha programu maalumu ya 2jiajiri lengo lake ni kuelimisha na kuwawezesha vijana kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi kama VETA na vituo vingine mbalimbali tukishirikiana karibu na serikali” Alisema Muro na kuongeza kuwa

“Tumeweza kuwafikia vijana zaidi ya 1780 na lengo ni kufikia zaidi ya hapo yaani vijana 5000 wengine ili waweze kupata hizi darasa na waweze kujiajiri wenyewe kuanzisha makampuni yao na kuajiri wengine”

Kadhalika Muro amesema lengo la kuanzisha program hiyo ni kuwainua vijana ili na wao baadae waweze kupata huduma za kibenki za kiislamu wakati wanataka kukuza biashara zao zaidi

Mbali na hayo, Muro amesema mteja akifungua account na KCB Sahal Banking fedha zake zitaenda kufanya shughuli ambazo ni halali lakini pia huduma zao wanazitoa kwa misingi ya sharia ambayo imekubaliwa na wanazuoni Tanzania nzima wa kiislam.

“Sisi kama KCB Sahal Banking kwakuwa ni dirisha ndani ya KCB Bank Tanzania, mahesabu yetu yote ziko tofauti kabisa na Zile zinazopokea riba, mtu akija kufungua account na KCB Sahal Banking inamaanisha zile fedha zako zinaenda kufanya shughuli ambazo ni halali kabisa na taarifa utaziona

Huduma tunazitoa kwa misingi ya sharia ambayo Imekubaliwa na wanazuoni Tanzania nzima wa kiislam” Alisema

Muro alisema wamejikita katika huduma za kimiamala, lakini pia huduma za account mbalimbali kama vile Current account, account za wanafunzi, watoto, na akaunti za kukusanya akiba pamoja na akaunti inayofanya vizuri ya vikundi isiyokuwa na malipo Wala Makato yoyote.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Sharia ya KCB Sahl Banking, Yasir Awadh aliwakaribisha wateja wote Sahal banking kwaajili ya kupata huduma mbalimbali za kibenki zenye kufata sharia za kiislam hasa katika uwekezaji na ukopeshaji wenye kufata maadili ya kiislam na pia uwekaji wa fedha ambao pia unafata maadili ya kiislam