Na Mwandishi Wetu

SHULE Kongwe ya Wavulana ya Sekondari Pugu imempongeza Bi.Maria Nyerere ambaye ni mjane wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kwa kumpa tuzo na zawadi mbalimbali lengo likiwa ni kuendelea kutambua mchango wa Mwalimu katika ukombozi wa Tanzania, Afrika kwa kwamba aliwahi kufundisha katika Shule hiyo.

Pongezi hizo zilitolewa Jijini Dar es Salaam  nyumbani kwa Bi. Nyerere na Mkuu wa Shule  hiyo Boniface Juma Orenda ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake ikizingatiwa Mwl. Julius Nyerere alifundisha shule hiyo na pia haikuishia hapo bali viongozi wengine ambao ni wakuu wa nchi waliendelea kutokana na matunda ya Pugu.

“Kwa kutambua mchango huu wa Hayati Mwalimu Nyerere, tumeona kuna umuhimu wa kuja kumuona mama yetu, kumjulia hali lakini na kutoa tuzo mbalimbali katika kutambua mchango wa bibi wa Taifa,” alisema Mkuu huyo wa Shule ya Sekondari ya Pugu Orenda.

Baadhi ya zawadi na tuzo mbalimbali zilizotolewa ikiwa ni pamoja na kumuenzi bibi wa Taifa.

“Kwa hiyo tumeona kama uongozi ni busara kumtembelea na kumpa tuzo na zawadi mbali mbali na kuendelea kuomba mambo mbalimbali ikiwemo ushirikiano kiano katika kuboresha kumbukumbu za hayati Mwalimu Nyerere na hasa kuhusu kwenye upande wa Taaluma, Imani pamoja na siasa.