Kampuni ya PARIMATCH imezindua kampeni yake kubwa ya Twenzetu Dubai na PARIMATCH, ikilenga kuwawezesha wateia wake wanaobashiri kupitia kampuni hiyo kwenda kutalii Dubai.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Levis Paul amesema kampeni hiyo ya cheza ushinde  itadumu kwa wiki nane  na kila wiki itatoa mtu mmoja na kumpeleka Dubai kutembea kwa siku nne.

“Wateja wapya hatujawacha anapojiunga kwa mara ya kwanza anapata bonasi ya shilingi 5000 hivyo cha kufanya ni kuscan QR code kwenye matangazo ya parimatch yaliyopo maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mabasi ya mwendokasi” Amesema Levis.

Katika hatua nyingine Kampuni ya Pari Match imemtangaza Mke wa Msemaji wa zamani wa Klabu ya Yanga,Zaylisa kuwa balozi mpya wa Kampuni hiyo pamoja na Vicenti Njau maarufu kama kiredio.

Aidha amesema wameamua kuchagua   mabalozi hao ili kuongeza ushawishi kwa watanzania kufuatilia Parimatch.

“Leo tunapenda kumtangaza Zaylisa kama balozi wetu na tumeingia naye mkataba kwani tuliona kwa ushawishi alionao asije kuchukuliwa na makampuni mengine, hivyo kuanzia Leo ni balozi wetu” Amesema na kuongeza kuwa,

“ tunafuraha kubwa sisi kama famili ya PARIMATCH inaongezeka, tumesaini mkmkatqba na vicent njau mnamfahamu kama. Kiredeo yeye atakuwa kama brand influencer”

Naye Haji manara Balozi mkongwe wa Parimatch amesema kampeni hiyo itawawezesha Watanzania kupata nafasi ya kwenda Dubai kwa safari ambayo imeshalipiwa kila kitu na Parimatch.

“Huko Dunia zamani walikuwa wanaeema kama hujaenda marekani, Paris bado hujasafiri lakini sasa hivi haitajwi tena sasa inatajwa Dubai ,ni mji bora zaidi sasa hivi Dunia unaulinzi wa hali ya juu”.