Aunty Ezekiel Grayson Jujuman; ni mwanamama wa Bongo Movies ambaye kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tetesi kuwa amekataliwa ukweli; yaani upande wa baba wa mtoto wake ambaye ni msanii Kusah.

Aunty anasema kuwa, ukweli ni kwamba familia ya Kusah inampenda kuliko hata Kusah mwenyewe anavyompenda.

“Yaani kuna wakati mpaka najiuliza sijui itakuwaje kwa sababu familia ya Kusah inanipenda kuzidi yeye (Kusah) anavyonipenda.

“Baba yake mzazi na mama yake ndiyo usiseme wanavyonipenda so sidhani kama kuna hivyo vitu. Hayo ni maneno tu au watu wanahisi hivyo, lakini hakuna kitu kama hicho,” anasema Aunty ambaye amezaa mtoto mmoja na Kusah.

Kwa upande wake Kusah anasema kuwa, hajawahi kuwa na mwanamke ambaye anakubalika kwenye familia yake kama Aunty.