Mheshimiwa Geophrey Pinda, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na pia ni Mbunge wa jimbo la Kavuu ametoa baiskeli mbili kwa watoto wenye ulemavu pamoja na kiasi cha shilingi Milioni Kumi Ili kuanzisha mfuko maalumu wa kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu.

Akiongea kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Usevya Mheshimiwa Pinda amesema “Ni lazima tuwasaidie watoto wetu kutimiza ndoto zao ikiwa ni pamoja na kuwasaidia katika mahitaji yao.

Aidha katika mkutano huo Mheshimiwa Pinda amewambia Wananchi kujitokeza kuhesabiwa ifikapo 23 Agosti 2022 kwani ni muhimu Sana kujua idadi yetu tumeongezeka wangapi”