Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhia ujenzi wa   barabara ya Kibada- Mwasonga-Kimbiji , ya kilomita 51 kujengwa kwa kiwango cha lami.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam leo na Waziri wa Ujenzi, Inocent Bashungwa katika ziara yake  kwa mkoa wa Dar es  Salaam kwa ajili ya kukagua miundombinu ya barabara  iliyoharibiwa na mvua.

“Rais wetu baada  kumpelekea taarifa ya changamoto ya barabara hii awali iliyoridhiwa kujengwa kwa kilomita 41,Rais  ameongeza ujenzi huo uwe wa kilomita 51,” amesema.

Amesema hatua iliyopo kwa sasa ni mkandarasi kupeleka mitambo ili mvua zitakapoisha aande ujenzi wa barabara hiyo mara moja.

Akizumngumzia mji wa Kigamboni amesema muhimu kwa sababu ni wa kibiashara na unatoa mchango mkubwa  hivyo aliwataka wananchi wa Kigamboni kutambua mvua zikiacha watajenga barabara zaa kudumu.

Amesema Serikali imejipanga kufanya tathmini  kuwa mvua zitakapoisha kurudisha miundombinu ya barabara ya kudumu hivyo  hakuna miundombinu itakayoharibiwa na mvua isirudishwe mawasiliano yake.

” Nimekuja kufanya ukaguzi wa barabara zilizoharibiwa na mvua  na kurudisha zoezi la uriudishaji wa mawasiliano ya muda ili kuwezesha shughuli za  uzalishaji  uchumi kuemndelea na mvua zikiisha  tutaendelea na matengenezo ya kudumu ya miundombinu  hii.

” Hakuna  barabara yoyote itakayokatika mawasiliano serikali ikashindwa kuyarejesha kwa sababu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya kurudisha miundombinu  iliyoharibiwa na mvua,” amesema.

Amesema maeneo  yeyete yenye mikwamo serikali iatawapeleka wakandarasi kurekebisha  kwa haraka iwezekanavayo.

Pia amesema Rais Dk. Samia  ameridhia ujemnzi wa   barabara ya Kibada- Mwasonga-Kimbiji , ya kilomita 51 kujengwa kwa kiwango cha lami.