KATIKA kuhakikisha wanakuza sekta ya Afya nchini Serikali imezindua miradi wa kuimarisha huduma za ukunga kwa mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga unaolenga kuwafikia wanawake milioni 1071,852 na watoto 805945 watakaojifungua katika vituo vya afya.

Miradi huo ni wa miaka saba kuanzia 2024-2030 ukifadhiliwa na serikali ya Canada kupitia shirika la Global Health Affairs Canada ukigharimu dola ya Canada 11, 750,000 ( sawa na Sh bilioni 22) ukiratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la afya na Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila amesema katika mikoa ya Dar es salaam na Shinyanga mradi utahusisha wilaya sita, za Shinyanga vijijini, Kahama, na Kishapu na Kwa Dar es Salaam ni eneo la Temeke, Ilala, na Kinondoni.
Aidha,Chalamila amesema jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 220 vitafikiwa na mradi huo, zahanati 180, vituo vya afya 28, na hospitali12, kata 28 na vijiji 112 vitafikiwa na mradi huu.

Ameongeza kuwa malengo makuu ya mradi ni pamoja na: kuongeza uwepo wa wauguzi wakunga wa kutosha na wenye ujuzi ili kuweza kupunguza magonjwa,
Kuboresha mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwa wakunga yanayozingatia usawa wa jinsia kwa watumishi walioko kazini na vyuoni.

” Hii pia itawaongezea ujuzi na weledi katika kutoa huduma za ukunga;Mradi pia utaangalia kuboresha ujuzi na weledi kwenye vyuo vya ukunga vya serikali ambapo wakunga wanazalishwa,” amesema na kuongeza ;pia mradi unalenga kuzingatia maswala mtambuka kama Kuzuia maambukizi ya Virusik vya ukimwi,Ukatili wa kijinsia, huduma rafiki kwa vijana na huduma zinazozingatia usawa, huduma za uzazi wa mpango kwa wasiofikiwa na njia hizo.