Katika kuhakikisha wanatunza mfumo wa Data, Wadau sekta ya Tehama wamezishauri taasisi zinazotumia mifumo hiyo ili kuongeza ufanisi zaidi ili kulinda taarifa zisidukuliwe na wahalifu wa mtandao.

Rai hiyo imetolewa leo mapema jijini Dar es Salaam na kampuni ya Dynatech Solutions wakishirikiana na kampuni ya Oracle kutoka Marekani.

Hivyo maofisa Tehama kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wameshauriwa kutumia mfumo wa kisasa utakaowezesha utendaji kazi mzuri wa uhifadhi wa taarifa za kiserikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tehama ya  Dynatech Solutions, Exaud Kimboi amesema ili kumaliza changamoto zilizopo mafunzo yanatolewa, elimu kwa watumiaji, ufahamu ili kuhakikisha teknolojia hizi zinaongeza ufanisi.

Hata hivyo,Kimboi,amesema Serikali inaagalia mahitaji ya teknolojia yaliyopo mbele hivyo tunaleta suluhisho ya mfumo huu.

“Kuna mabadliko ya mifumo ya Tehama na tumeshauri namna ya kubadili mifumo hiyo bila ya kuleta athari. Serikali inatakiwa ikae na wataalamu wao wa Tehama na binafsi wawape mahitaji yatakayokidhi wakati husika na wakati ujao,” amebainisha.

Mtaalamu huyo,Ameonggeza kuwa lazima iwepo mifumo ya kisasa yenye kukidhi mahitaji ya kihuduma ambapo faida yake ni kuokoa muda kwa watumiaji na hata wananchi.

Kwa upande wake,Majaliwa John,ambaye ni Ofisa Tehama kutoka Wakala wa Majengo Nchini TBA, amesema katika dunia ya sasa mifumo ya uhifadhi taarifa yenye usalama na uhakika ndio inayohitajika.

Akitolea mfano taasisi anayotoka amesema taarifa zao zinazohusu ujenzi na usanifu lazima uwepo mfumo mzuri ambao utatunza taarifa hizo sambamba na kuingiliana na mifumo mingine. Hivyo uelewa utakaopatikana leo ni muhimu.

Kwa upande wake Ofisa Tehama kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra), Kevin Kituli amesema matarajio yake baada ya kupata ujuzi ataendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

“Mfano suala la ulinzi ni la muhimu kupata elimu kila wakati ili kutunza taarifa jambo ambalo ni changamoto sehemu nyingi duniani,” amesema Kituli.

Moses Mwangi, Meneja Uhasibu taasisi za Serikali Afrika Mashariki kutoka Kampuni ya Oracle amesema taasisi za Serikali pamoja na binafsi zinapaswa kujiimarisha zaidi katika matumizi ya mfumo mpya na wa kisasa.