Kampuni ya Selcom pamoja na Nala zimeingia makubaliano ya Ushirikiano ya kuongeza nguvu ya kutuma fedha nchi za nje kutoka Uingereza na Marekani moja kwa moja kuja Tanzania kupitia simu za mikononi na Akaunti za Benk.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiliaji saini huo Mkurugenzi mtendaji wa Selcom,Sameer Harji ,amesema wanafuraha kushirikiana na Nala kampuni ambayo inamilikiwa na mtanzania.

“Ushirikiano wetu utawawezesha wateja wa Nala kutuma pesa kwa njia ya uwazi na Ufanisi ,hivyo kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya wateja wa Nala nchini Tanzania na kuunda njia mpya ya utumaji fedha kwa watu wanaoishi nje ya Afrika kuja Nyumbani na kwa msaada wa Benki kuu na washirika kama vile NALA”
Amesema Hirji.

Naye mwanzilishi na Mkuregenzi Mtendaji wa Nala,Benjamin Fernandes amesema ushirikiano na Selcom ni ishara ya kuimarisha uwepo wa Nala katika masoko waliyopa kipaumbele.

“Afrika ndio bara ghali zaidi duniani kutuma pesa,na lengo la Nala ni kubadilisha dhana hiyo kwa kuunda masuluhisho ya Kifedha ambayo waafrika wanastahili,na tunapozidi kupanua bidhaa zetu ili kuwafikia watu wengi zaidi,inakuwa muhimu zaidi kupata washirika muhimu ili kutimiza azma hiyo.”Ameongeza kusema Fernandes.