ALIYEKUWA Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa nyakati tofauti,Boniface Jacobo, amewashauri wananchi wa mkoa Dar es Salaam kususia kulipia ushuru wa halmashauri tano za mkoa huo mpaka pale watakapochukuliwa hatua waliohusika na wizi wa fedha za halmashauri hizo zilizoibuliwa kwenye Ripoti ya Mzibithi na mkaguzi wa mahesabu za serikali(CAG).

Jacob ametoa Rai hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akichambua ya Ripoti ya CAG kwenye halmashauri tano za mkoa wa Dar es salaam.

Aidha,Jacobo amesema kupitia Ripoti hiyo imeonesha ufisadi mkubwa kwenye halmashauri ya Ubungo,Halmashauri ya jiji la Dar es salaam pamoja na kigamboni .

“Natoa rai kwa wakazi wote wa Dar es salaam kususia kulipa ushuru zote za manispaa ,haiwezekani watanzania walipe ushuru halafu pesa zinaliwa na wajanja kwenye hizi halmashauri”Amesema Jacobo.

Ameongeza kuwa atatumia nafasi yake ya uanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kuitisha mikutano ya hadhala mkoa wa Dar es salaam kuwahimiza wananchi na wakazi wake kususia kulipa ushuru mpaka wahusika wachukuliwe hatua.

Kadhalika,Jacobo amesema katika Ripoti ya CAG kumeonesha ufisadi mkubwa ikiwemo kupoteza fedha za miradi,fedha za mikopo kwa vijana,kuchelewa kwa miradi.

Pamoja na hayo Jacobo amesema hatua alizochukua Rais wa Jamhuri wa Muungano,Samia Suluhu Hassani,kuhusu wahusika waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG na kusema hatua hiyo ni ndogo kwani hatua zaidi zinahitajika.