Benki ya biashara Tanzania (TCB) imeendelea kutoa mikopo kwa wastaafu ambapo hadi sasa wametoa takribani bilioni 700 kwaajili ya kundi hilo ambalo limetumikia nchi katika nyanja mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB Bw.Adam Mihayo wakati akizungumza katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa hazina,jukwaa la wahariri Tanzania kilichofanyika leo Aprili 9, 2024 kwenye hotel ya Hyyat Regency Jijini Dar es salaam.

Amesema wao ndio walianzisha mikopo kwa wastaafu maana waliona wanapomaliza muda wao kazini taasisi nyingi za fedha zinawasahau katika kuwakopesha hivyo wakaja na mfumo ambao umeliwezesha kundi hilo kupata mikopo.

Aidha, ameeleza kuwa Kwenye upande wa huduma za kidijitali wamefanya mwingiliano na sisitimu mbalimbali ikiwemo TRA,GPG,EMS ili kuwawezesha wateja wao kufanya miamala mbalimbali na Serikali na taasisi za kiserikali.

“Tunafanya utaratibu wa kulipa mishahara kwa wafanyakazi,kama Kampuni inataka kupitisha mishahara kwetu hiyo huduma tunayo pia kupitia huduma hiyo tunaweza kutoa mikopo kwa wafanyakazi”,amesema Mihayo

Ameeleza kuwa kwenye upande wa mapato wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na taasisi kuaminika na kwa mwaka Jana mapato yalikuwa bilioni 184.

Amesema Amana ndio kiashiria kikubwa cha kuaminiwa na wateja pia tumekuwa tukipiga hatua ambapo mwaka jana zimekuwa kwa asilimia 11.

“Upande wa mikopo pia tumekuwa tukikuwa mwaka hadi mwaka na kwa mwaka jana tumefunga na bilioni 916 sawa na asilimia 9 na mwaka huu tunamkakati wa kukuza zaidi sekta ya wafanyabiashara na tayari tumetenga bilioni 300 kwaajili ya kuwasapoti”,

Amesema wakiisaidia sekta hiyo kutakuwa na ongezeko la ajira na itasaidia kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa Serikali.

Akizungumzia mali zao amesema mwaka Jana walifunga na tilioni 1.4 na kwa mwaka huu wanahitaji kukua hadi tilioni 1.7 kwani uwezo huo wanao.

Mwisho ameeleza kuwa mwaka jana walifunga na tilioni 120 huku akiishukuru Serikali kwa kuyaongezea mtaji.