Mwenyekiti wa Jukwaa la mwanahabari wa Mtandao wa kijamii Tanzania (JUMIKITA ) Shabani Matwebe amelaani na kukemea matusi yanayoendelea katika mitandao ya kijamii yanayomzalilisha mwanamke.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Matwebe amesema  baada ya kukaa kikao  na kuona kwamba kuna matatizo makubwa ambayo sasa ni kama Tabia mpya imezuka kwenye mitandao ya kijamii, badala ya kujadili hoja, sasa kwenye mitandao yanajadiliwa matusi.


Amesema matusi yanayoendelea si kitendo cha kiungwana, matusi yanayojadiliwa mengi ambayo sasahivi yameshika hatamu ni kwamba mwanamke amekuwa mtu wa kutwezwa utu wake.


“Kwenye mitandao panapotokea matusi ya kuondoa utu wa mtu kwa namna ambavyo heshima na utu wake unavyotwezwa kutokana na kafsha au kebehi au dhalilishaji maana yake sisi kama taaisisi tuna wajibu wa kutoa mawazo yetu”, amesema Matwebe.



Amesema leo Dunia nzima inapambana namna ya kumlinda mwanamke, na hakuna namna ya kulifanikisha jambo hili kama kwa kauli Moja tukikubaliana kwamba tujadili hoja, tuikosoe serikali, tuseme mahitaji ya wananchi, tuseme changamoto za wananchi ili serikali ichukue hatua.




Amesema  Sisi kama Taasisi tumeona tuna mambo makuu mawili, ikiwemo kukemea, kuendelea kunyamaza kimya ni kwamba tunaendelea kufanya jambo liendelea pasipo na msingi maalumu.



Amesema Serikali mwaka huu inaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu, wapo watu mbalimbali watagombea wenye jinsia ya kike, kama leo hii watatwezwa na kudhalilishwa, nani mtoto wa kike atapata ujasiri wa kwenda kuchukua fomu,? anasimamaje jukwaani kusema chochote!”.


Aidha amevitaka vyombo na tasisi zote zinazotetea masuala ya wanawake kuacha kukaa kimya na badala yake wakemee na kulaani matusi ya mwanamke mwenzao kwa kuwa kukaa kimya kwao kuna maslahi wanayoyapata na matusi hayo.